Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Msemaji wa Jeshi la Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Akrami-Nia, amesema kuwa mfumo uliopo chini ya ushawishi wa Iran katika Mlango wa Hormuz hauwezi kurejeshwa nyuma, akisisitiza kuwa Marekani haina chaguo jingine isipokuwa kuukubali hali hiyo.
Akizungumza katika mkusanyiko wa wananchi mjini Tehran, Brigedia Jenerali Akrami-Nia amesema kuwa endapo Marekani itakataa kukubali hali iliyopo, italazimika kukabiliana na gharama ambazo zitakuwa kubwa zaidi kuliko gharama ilizowahi kubeba hapo awali.
Brigedia Jenerali Akrami-Nia pia ameangazia athari za ushiriki mkubwa wa wananchi katika mikusanyiko ya usiku, pamoja na uungaji mkono wao mpana kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Amesema kuwa miongoni mwa matokeo muhimu ya uwepo mkubwa wa wananchi katika mikusanyiko hiyo ni kufifisha njama za maadui zinazolenga kuuangusha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na kuimarisha ari, hamasa na morali ya wananchi wa Iran katika kulinda nchi yao na mfumo wa Kiislamu.
Aidha, amesema kuwa mshikamano na uwepo wa wananchi katika mikusanyiko hiyo unatoa ujumbe wa wazi wa kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu na kuimarisha dhamira ya vikosi vya jeshi la Iran katika kuilinda nchi hiyo.
Maoni yako